Nkomola amshawishi Lwandamina

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
13 Jan 2018
Nkomola amshawishi Lwandamina
Donald Ngoma na Amissi Tambwe wamekosekana kwa muda mrefu ndani ya kikosi cha Yanga kutokana na kuwa majeruhi na kuwapa presha Wana Jangwani.

Lakini kocha George Lwandamina ametumia dakika 90 kugundua kitu kwa straika mpya chipukizi Yohana Nkomola na kutamka; “Huyu akitulia anakinisikiliza atakuwa Ngoma mpya.”

Nkomola aliyesajiliwa na Yanga kwenye dirisha dogo akitokea kikosi cha Timu ya Taifa ya Vijana U17, amemkuna mno Mzambia huyo na kudai kama akituliza akili akawasikiliza makocha wake atakuwa ni mwiba mkali uwanjani.

Katika mahojiano na gazeti la Mwanaspoti, Lwandamina aliyeamua kukaa jukwaani katika mchezo wa mwisho kati ya Yanga dhidi ya URA na timu yake kung'olewa michuano ya Mapinduzi kwa matuta, aligundua kuwa Nkomola ni moja ya kipaji bora walichonacho katika safu yao ya ushambuliaji.

Alisema Nkomola ni moja kati ya usajili bora waliowahi kuufanya ambapo, kama ataendelea kuwa msikivu na kudumisha nidhamu atakuwa na bonge la mchezaji katika kikosi hicho kwenye michezo ya Ligi Kuu na hata kimataifa.

Alisema kinda huyo anaonekana kuwa na makali ikiwemo kasi akiwa pia na ubora wa kujua kujitenga katika maeneo mazuri ya kufunga, lakini anahitaji kuongezewa vitu vichache tu.

“Angalia akitoa pasi anachofanya hazubai anakimbilia sehemu sahihi kusubiri afunge, pia anapenda kuhakikisha kama hapa kipa kashadaka au nafasi imepotea ni moja kati ya vipaji bora tumevipata,” alisema Lwandamina.

“Ukiwa kocha sio kila wakati utapata mchezaji aliyekamilika kuna vitu vimepungua kwake nitapambana kumbadilisha taratibu, lakini naamini kama akiwa msikivu na akidumisha nidhamu nitamfanya kuwa mchezaji bora katika safu ya ushambuliaji.

“Uwezo wake ni kama alionao Ngoma, ambaye kwa muda mrefu amekuwa nje ya uwanja, ila Nkomola akikaa sawa atafukia mashimo yote ya safu ya ushambuliaji.”
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →