Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' jioni ya leo itashuka uwanjani Madagascar katika mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya kombe la Dunia
Mchezo huo utakaopigwa kuanzia saa kumi Alasiri, ni wa kukamilisha ratiba kwani timu zote zimeshaondoshwa mashindanoni
Benin na DR Congo zitachuana katika mchezo mwingine ambao utaamua ni timu ipi inavuka raundi ya tatu
DR Congo wanahitaji ushindi wakati Benin wanahitaji alama moja tu katika mchezo huo utakaopigwa Lubumbashi DR Congo
Tanzania ilitua Madagascar juzi wakisafiri na ndege binafsi (ATCL) ambayo itawarudisha nyumbani baada ya mchezo huo
ADVERTISE HERE