Usiku wa jana ilifanyika hafla maalum ya kumpongeza Rais Dr. HUSSEIN ALI MWINYI kwa kutimiza mwaka mmoja wa uongozi wake kwenye serikali ya awamu ya nane ZANZIBAR.
Katika hafla hiyo iliyo sheheni maafisa waandamizi wa Serikali ikiongozwa na Mh. Dr. MWINYI, Makamu pili wa Rais Zanzibar Mh. HEMED SULEIMAN ABDULLA, Mawaziri, Mabalozi na WADHAMINI, WAFADHILI na WAHISANI wa Serikali ya Zanzibar.
Hafla hiyo maalum iliyoandaliwa na WIZARA YA MICHEZO ( ZANZIBAR ) ililenga kumpongeza Rais MWINYI na serikali yake lakini pia kuwashukuru na kutambua mchango wa wadau mbali mbali katika sekta ya michezo.
"Ama hakika, katika maendeleo ya michezo nchini UDHAMINI ndio nguzo kubwa. Nakuagiza WAZIRI wa michezo utoke ukatafute wadhamini ili tuweze kupata ligi iliyo bora"
"Leo nakupongeza Mh. Waziri kwa kuweza kukusanya zaidi ya milioni 900 Tsh kutoka kwa wadhamini mbalimbali," alisema Dr. Hussein Mwinyi
GSM ilikuwa na sehemu ya kutambuliwa kwa mchango wake katika UDHAMINI wa LIGI KUU visiwani Zanzibar
"Ninayo furaha kupokea HATI YA SHUKRAN kutoka kwa RAIS wa ZANZIBAR na Mwenyekiti wa BARAZA LA MAPINDUZI, Mh. Dr. HUSSEIN ALI MWINYI. Aidha, GSM itaendelea kuwa sehemu kubwa ya kuchangia maendeleo ya michezo nchini kwetu tukiamini mchango huu unakwenda kugusa moja kwa moja maisha ya vijana wetu wenye vipaji," alisema Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Injinia Hersi Said