Waliokuwa timu za Taifa kuanza kurejea leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Nov 2021
Waliokuwa timu za Taifa kuanza kurejea leo

Wachezaji wa Yanga waliokuwa na majukumu ya timu za Taifa, wanatarajiwa kuanza kurejea kikosini leo baada ya kukamilisha majukumu hayo

Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' ilikuwa na wachezaji sita wa Yanga ambapo Stars ilirejea nchini jana baada ya mchezo dhidi ya Madagascar uliomalizika kwa sare ya bao 1-1

Feisal Salum, Kibwana Shomari na Dickson Job walikuwa sehemu ya kikosi kilichoanza mchezo dhidi ya Madagascar wakati Bakari Nondo Mwamnyeto alikuwa miongoni mwa wachezaji waliowekewa ngumu na wenyeji kucheza kwa kisingizio cha maambukizi ya covid 19

Pia katika kikosi hicho walikuwemo Ramadhani Kabwili na Zawadi Mauya

Khalid Aucho aliingoza timu ya Taifa ya Uganda kwenye mchezo dhidi ya Mali ambayo yupo mlinda lango Djigui Diarra, mchezo huo ukimalizika kwa Mali kushinda bao 1-0

Shabani Djuma alikuwa sehemu ya kikosi cha DR Congo kilichoichapa Benin mabao 2-0 na hivyo kutinga hatua ya mtoano kusaka tiketi ya fainali za kombe la Dunia

Mkongwe Saido Ntibazonkiza yeye aliitwa timu ya Taifa ya Burundi ambayo ilicheza mechi za kirafiki

Nyote hao wanarejea sasa kuendelea na mikiki mikiki ya ligi kuu ambapo mwishoni mwa wiki hii Yanga itashuka uwanjani kule Ilulu, Lindi kuikabili Namungo Fc

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’