Kikosi cha Yanga sasa kitaondoka jijini Dar es salaam kesho asubuhi kuelekea Lindi wanakokabiliwa na mchezo wa ligi kuu dhidi Namungo Fc utakaopigwa uwanja wa Ilulu
Msemaji wa klabu ya Yanga Haji Manara amesema kikosi kitaondoka Alhamisi asubuhi kuelekea Lindi
Manara amesema ni wachezaji wawili tu ambao watabaki jijini Dar es salaam wakiendelea na program maalum za mazoezi ili kuimarisha afya zao
"Tunakwenda Lindi tukiwa na kikosi kamili. Wachezaji wanaobaki Dar ni Mapinduzi Balama na Dickson Ambundo ambao wanaendelea na program maalum za mazoezi"
"Tunajua hautakuwa mchezo mwepesi, tunakwenda kucheza na Namungo Fc ambao wako nyumbani lakini naamini tutatimiza lengo la kuondoka na ushindi"
"Wachezaji waliokuwa na majukumu ya timu za Taifa wengine wamesharejea, Djigui amewasili Alfajiri ya leo wakati Shabani Djuma na Khalid Aucho watawasili kesho na moja kwa moja kuunganisha Lindi," alisema Manara
Kikosi kitaondoka kesho kuelekea Lindi tayari kwa mchezo wetu wa Ligi Kuu NBC dhidi ya Namungo Fc, Jumamosi ya tarehe 20/11/21 kwenye Uwanja wa Ilulu.
— Young Africans SC (@yangasc1935) November 17, 2021
Shabiki wa Young Africans Lindi na Mikoa ya jirani huna sababu ya kukosa burudani na Pira ????????????@HajiManara pic.twitter.com/KYgfV9ChRO