Tuko tayari kuikabili Namungo Fc - Nabi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Nov 2021
Tuko tayari kuikabili Namungo Fc - Nabi

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, amesema malengo yao ni kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Namungo FC 

Kikosi cha Yanga kilitua mkoani Lindi jana jioni ambapo Nabi alibainisha kuwa wachezaji wake wote waliosafiri na timuwako fiti na anatarajia watafanya kile ambacho amekieleza kwenye programu zake mbalimbali.

Nabi amebainisha kuwa kila mchezaji amempa majukumu yake na amewataka wawe na 'heshima' kwa wapinzani wao kwa sababu wanacheza ugenini.

"Tumeshakamilisha programu za mazoezi kwa ajili ya mechi yetu ya Jumamosi, kilichobakia ni maelekezo madogo madogo, katika mpira huwezi kumaliza mechi mpaka utakaposikia filimbi ya mwisho, kwa sasa tunaiangalia kwa awamu ya mwisho kabla ya kuingia uwanjani," alisema Nabi

Ni mchezo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali kutoka kwa kila timu, rekodi za michezo ya nyuma zikidhihirisha hilo

Namungo Fc tangu ilipopanda daraja misimu miwili iliyopita, michezo yake yote dhidi ya Yanga ilimalizika kwa matokeo ya sare

Ushindi pekee waliopata Yanga ni kwenye michuano ya kombe la FA msimu wa 2018/19 wakishinda bao 1-0, bao la Heritier Makambo

Nabi ataingia katika mchezo huo akikumbuka matokeo ya msimu uliopita walipolazimishwa suluhu ya bila kufungana katika mchezo ambao bao la Yacouba Songne lilikataliwa na mwamuzi msaidizi aliyefungiwa baada ya mchezo huo

Yanga imeweka malengo makubwa ambapo Wananchi wanautaka ubingwa wa ligi kuu walioupoteza kwa msimu minne mfululizo kwa watani zao Simba

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’