Kiungo wa Yanga Khalid Aucho anaendelea kujiiimarisha nchini Uganda kabla ya kurejea nchini kuendelea na majukumu yake ndani ya kikosi cha Yanga
Aucho alipata majeraha kwenye mchezo wa kuwania kufuzu kombe la Dunia dhidi ya Mali na hivyo kukosa mchezo uliopita dhidi ya Namungo Fc
Daktari huyo wa mpira amekosa mechi mbili mfululizo za ligi kutokana na changamoto za majeraha
Kabla ya mchezo dhidi ya Mali, alikosa mchezo dhidi ya Ruvu Shooting baada ya kuumia mazoezini
Kocha Nasreddine Nabi anaweza akaendelea kumpa mapumziko kumuandaa kwa ajili ya mchezo dhidi ya Simba ambao utapigwa Disemba 11
Aucho ana kadi mbili za njano, kama atatumika katika mchezo ujao dhidi ya Mbeya Kwanza na akapata kadi ya njano, maana yake ni kuwa atakosa mchezo dhidi ya Simba
