Baada ya mapumziko ya siku mbili, kikosi cha Yanga kinarejea kambini leo kuanza maandalizi ya mchezo wa ligi kuu ya NBC dhidi ya Mbeya Kwanza
Mchezo huo wa raundi ya saba, utapigwa wiki ijayo, Novemba 30 uwanja wa Sokoine, Mbeya
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema baada ya timu kurejea Dar kutoka Lindi walikolazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Namungo Fc, Kocha Mkuu Nasreddine Nabi alitoa mapumziko ya siku mbili
Bumbuli amesema kikosi leo asubuhi kinaanzia Gym kabla kuelekea Avic Town kwa ajili ya mazoezi ya mazoezi mengine
ADVERTISE HERE