Kiungo Mapinduzi Balama 'kipenseli' kwa sasa amepona majeraha yaliyomuweka nje kwa zaidi ya mwaka mmoja baada ya kuvunjika mguu mwishoni mwa msimu wa 2019/20
Balama amemaliza program binafsi za mazoezi alizokuwa akifanya ili kurejesha utimamu wake wa mwili na sasa madaktari wamejiridhisha yuko 'fit' na kumkabidhi kwa benchi la ufundi kuweza kumtumia
Pamoja na Balama, Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema winga Dickson Ambundo aliyekuwa akisumbuliwa na tatizo la mkono, nae amepona kama ilivyo kwa Yassin Mustafa ambaye alipata nafasi ya kucheza kule Visiwani Zanzibar

Bumbuli amesema wachezaji wote wataingia kambini leo na wenzao na watakuwa na nafasi ya kumshawishi Nabi kuweza kuwajumuisha katika kikosi chake
Mashabiki wa Yanga wana shauku ya kumshuhudia Balama baada ya kutomuona uwanjani kwa zaidi ya mwaka mmoja
Ni suala la muda sasa, Balama ataonekana katika kikosi cha Yanga