Kiungo kiraka wa Yanga Yannick Bangala atakosa mchezo ujao wa ligi kuu dhidi ya Mbeya Kwanza akitumikia adhabu ya kadi tatu za njano
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amethibitisha adhabu ya Bangala lakini amesema hakuna wasiwasi kwa sababu anao wachezaji wanaoweza kutumika katika eneo lake
"Nikweli tutamkosa Bangala katika mechi ijayo lakini bado tuna watu wa kuziba nafasi yake na tukacheza kwa ubora wetu,hiyo ni mechi ambayo tunahitaji ushindi kwa nguvu yetu"
"Tutamkosa katika mecho hii dhidi ya Mbeya kwanza lakini tuna uhakika wa asilimia mia moja tutakuwa naye katika mchezo utakaofuata dhidi ya Simba," alisema Nabi
Aidha Nabi amesema Khalid Aucho amerejea na watamuangalia kama wataweza kumtumia katika mchezo huo utakapigwa Novemba 30
"Aucho anaweza kurejea ameanza mazoezi vizuri lakini bado tutamfuatilia maendeleo yake kama ataweza kuwa tayari kwa mchezo ujao au tuwe na mpango gani mpya,hayo yote tutayafanyia uamuzi kabla ya kuelekea Mbeya"
Aucho pia ana kadi mbili za njano, ni wazi Nabi atahitaji kumtumia kwa tahadhari kwenye mchezo dhidi ya Mbeya Kwanza kwani kama atapata kadi atakosa mchezo dhidi ya Simba
Huenda ikawa nafasi kwa kiungo Zawadi Mauya kurejea kikosini sambamba na Mukoko Tonombe ambaye amehusika katika michezo miwili iliyopita