Achana na usajili makini ambao umewezeshwa na GSM kuifanya Yanga kuwa na kikosi bora msimu huu
Pale kwenye benchi la ufundi kuna watu wawili ambayo wamebeba hatma ya furaha ya Wananchi
Profesa Nasreddine Nabi, Kocha Mkuu na Cedric Kaze, kocha msaidizi
Hawa watu ndio wanachora ramani ya mafanikio ya Yanga msimu huu
Umekuwa mwanzo mzuri kwao, timu inaongoza ligi baada ya kushinda mechi tano na kutoka sare mchezo mmoja
Lakini muhimu zaidi wameunda timu ambayo haipati ushindi kwa kubahatisha, soka linalopigwa na wananchi hasa wakiwa kwenye ubora wao linaogofya!
Makocha hawa wakiendelea kuaminiwa na kupewa sapoti na uongozi, wanachama na mashabiki, hakuna shaka msimu huu ubingwa utapatikana
ADVERTISE HERE