Baada ya kumalizika kwa michuano ya kombe la Mapinduzi, kikosi cha Yanga kimerejea rasmi mazoezini kujiandaa na michezo ya ligi kuu ya Vodacom pamoja na michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika.
Yanga ilianza rasmi mazoezi jana Jumapili asubuhi kujiandaa na mchezo wa ligi unaofuata dhidi ya Mwadui FC siku ya keshokutwa Jumatano, Januari 17.
Kocha George Lwandamina aliongoza mazoezi hayo kwa mara ya kwanza baada ya kukosekana kwa zaidi ya mwezi kutokana na matatizo yaliyomkumba ya kufiwa na mwanawe nchini Zambia.
Michuano ya kombe la Mapinduzi imeinua ari ya wachezaji wa kikosi cha Yanga ambao wameapa kuisambaratisha Mwadui FC kwenye dimba la Uhuru keshokutwa.
Aidha kurejea mazoezini kwa kiungo Thabani Kamusoko na mshambuliaji Donald Ngoma kumeongeza 'utamu' wa kikosi cha Yanga.
Kocha George Lwandamina amesema baada ya kuridhishwa na viwango vya baadhi ya wachezaji, analazimika kukifumua kikosi chake cha kwanza.
Lwandamina amesema anafurahishwa zaidi na ushindani wa namba uliopo sasa kwani utainufaisha klabu kwa kuwa hakuna mchezaji mwenye uhakika kama atacheza mchezo unaofuata.

ADVERTISE HERE