Kiungo fundi wa Yanga Khalid Aucho amesema haizingatii mijadala inayoendelea kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu yeye ni mchezaji wa Yanga akiwa na mkataba wa miaka miwili
Aucho amesema yeye ni mchezaji wa kulipwa ambaye anaheshimu mikataba hivyo Wanayanga hawapaswi kuwa na wasiwasi
"Mkataba wangu na GSM wanaufahamu, mimi ni mchezaji wa Yanga kwa misimu miwili, mashabiki wa Yanga hawapaswi kuwa na wasiwasi kwani siendi popote"
"Kama nikimaliza mkataba naweza kuwakaribisha lakini kwa sasa mimi ni mchezaji wa Yanga kwa miaka miwili," alisema Aucho
ADVERTISE HERE