Yanga yasaka mbadala wa Yacouba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Nov 2021
Yanga yasaka mbadala wa Yacouba

Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Injinia Hersi Said ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, amesema wameanza mchakato wa kusaka mshambuliaji ambaye ataziba nafasi ya Yacouba Songne aliyepata majeraha ambayo yatamuweka nje kwa muda mrefu

Hersi amesema tayari wana mapendekezo ya wachezaji akiamini hadi kufikia dirisha dogo mshambuliaji huyo atakuwa amepatikana

"Tayari tumeshaingia kazini kutafuta mchezaji wa kuziba pengo la Yacouba Songne aliyepata majeraha ambayo yanaweza muweka nje hadi mwisho wa msimu. Tayari tuna mapendekezo nafikiri wakati mwafaka utakapofika kila kitu kitafahamika," alisema Hersi

Aidha kumekuwa na tetesi nyingi kumuhusu kiungo wa zamani wa Simba Clatous Chama ambaye inaelezwa kuwa ameomba kuvunja mkataba wake ya RS Berkane anayoitumikia sasa huku kukiwa na taarifa Wakala wake alikuwa nchini hivi karibuni ambapo alipata nafasi ya kuonana na 'Bosi wenyewe' GSM

Hersi amesema suala la mchezaji huyo linazungumzwa zaidi kama tetesi hivyo ni vyema likaendelea kubaki hivyo hivyo kama kutakuwa na jambo lolote litafahamika huko mbeleni

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
2h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
3h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
6h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
21h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’