Tetesi za kiungo Salum Abubakar 'Sure Boy' kuelekea kwa Wananchi zimeanza tena zikiwa zimesalia wiki mbili kabla ya dirisha dogo la usajili kufunguliwa
Kiungo huyo mwandamizi katika kikosi cha Azam Fc, kwa sasa yuko nje ya uwanja baada ya kusimamishwa kwa muda usiojulikana akikabiliwa na tuhuma za utovu wa nidhamu
Hata hivyo Sure Boy na wenzake Mudathir Yahya na Agrey Morris wamepeleka malalamiko yao TFF wakipinga kifungo hicho kisicho na ukomo. Wanaitaka Azam Fc kuvunja mikataba yao kama hawawahitaji tena
Katika dirisha la usajili lililopita, Yanga ilipeleka maombi ya kumsajili Sure Boy kwa klabu yake ya Azam lakini wanaramba ramba hao wakaigomea ofa ya Yanga licha ya kuwa Sure Boy mwenyewe alikuwa tayari kujiunga na Yanga
Yanga inatarajiwa kukiimarisha kikosi chake kwenye usajili wa dirisha dogo litakalofunguliwa Disemba 15
Nafasi ya kiungo mshambuliaji ambayo hucheza SureBoy ni miongoni mwa maeneo ambayo Yanga imepanga kuyaimarisha