Mtendaji Mkuu wa Yanga Senzo Mazingisa amewataka Wanachama na Mashabiki wasikubali kuvurugwa na taarifa za kupikwa mitandao wakati huu kuelekea mchezo dhidi ya Simba ambao utapigwa Disemba 11 katika uwanja wa Benjamin Mkapa.
Mara nyingi mchezo wa watani wa jadi ukikaribia, huibuliwa mambo mengi ya uchonganishi huko mitandao lengo likiwa kuondoana mchezoni
Senzo amesema amezisikia taarifa zinazosambazwa mitandao zikidai kocha Mkuu Nasreddine Nabi na kocha Msaidizi Cedric Kaze hawaelewani jambo ambalo halina ukweli wowote
"Hakuna hicho kitu nilishangaa zaidi hali ambayo nimeikuta kambini, kinachofanyika kule ni ushirikiano kwa watu wote ili tushinde hizi mechi mbili na zingine zijazo hakuna kingine, unapoona hizi taarifa unalazimika kucheka," alisema Senzo
Senzo amesema msimu huu wamedhamiria kutimiza adhma yao ya kutwaa ubingwa hivyo wamejipanga kupambana na fitna zote zinazoanzishwa kwa lengo la kuwaondoa katika mipango yao
Amesema baada ya mchezo dhidi ya Mbeya Kwanza, timu itarejea jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo dhidi ya Simba ambao wamepania kushinda