Kikosi cha Yanga kilirejea jana kutoka mkoani Mbeya ambako walifanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya Kwanza
Baada ya timu kurejea Dar, uongozi ulitoa mapumziko ya siku mbili kwa wachezaji kwenda kuziona familia zao kabla ya kurejea kuanza maandalizi ya mchezo dhidi ya Simba ambao utapigwa Disemba 11 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Yanga Senzo Mazingisa amesema baada ya mapumziko hayo kikosi kitarejea kambini kuanza maandalizi ya mchezo huo
"Tumeona wachezaji nao wakazione familia zao katika hizi siku mbili na baada ya mapumziko hayo tutarejea kazini kuanza kujipanga na mchezo huo unaokuja dhidi ya watani wetu Simba," amesema Senzo
"Sio viongozi, wachezaji na hata benchi la ufundi sote tunajua umuhimu wa ushindi kwahiyo tutakuwa na maandalizi yanayolingana na uzito wa hii mechi tunakiamini kikosi chetu"