Tume ya Ushindani wa Biashara (FCC) imesema imepokea malalamiko kutoka kwa wadau wa mpira wakiitaka kuchunguza udhamini uliofanywa na kampuni ya GSM kwa Ligi Kuu ya NBC Tanzania kama hautaathiri ushindani wa soka nchini
Wadau hao wamewasilisha malalamiko yao kwa maandishi ndani ya tume hiyo Jumatatu ya Novemba 29, 2021 wiki hii kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa FCC, William Erio wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Malalamiko hayo yamepokelewa ikiwa ni siku chache tangu kampuni ya GSM kusaini mkataba wa Sh2.1 bilioni na Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF)
Udhamini huo utazinufaisha klabu zote 16 zinazoshiriki ligi kuu ya NBC
ADVERTISE HERE