Wakati mshambuliaji Ditram Nchimbi akiwa tayari amejiondoa kikosini akisubiri mkataba wake umalizike ili ajiunge na Geita Gold, kuna wachezaji wengine atamfuata kwenye usajili wa dirisha dogo
Baadhi ya wachezaji mikataba yao inamalizika na Kocha Mkuu Nasreddine Nabi ameonekana kutokuwa na mahitaji nao
Adeyum Saleh, Ramadhani Kabwili na Paulo Godfrey 'Boxer' wanatajwa kuwa katika mpango huo
Usajili wa dirisha dogo utafunguliwa wiki ijayo, Yanga ikitarajiwa kukiboresha kikosi chake kwa kuimarisha maeneo yenye mapungufu
Aidha Yanga inatarajiwa kusajili nyota wengine wawili wa kigeni ambao nafasi moja ni mshambuliaji na mwingine ni kiungo
Baada ya Yacouba Songne kupata majeraha ambayo yatamuweka nje mpaka mwishoni mwa msimu, Yanga inaleta mshambuliaji wa kuziba nafasi yake