Feisal, Yannick, Aucho na Mayele watasumbua sana - Mtemi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Dec 2021
Feisal, Yannick, Aucho na Mayele watasumbua sana - Mtemi

Wakati joto la pambano la watani Simba na Yanga likiongezeka, nyota wanne wa Yanga wametajwa kuwa mwiba kwa Simba kwenye mchezo huo wa dabi

Nyota hao ni Feisal Salum, Yannick Bangala, Khalid Aucho na Fiston Mayele ambao wametajwa na mchezaji wa zamani wa Simba, Mtemi Ramadhan akisema watakuwa kikwazo kwenye timu yake hiyo ya zamani kwenye dabi hiyo ya kwanza kwenye Ligi Kuu Tanzania bara msimu huu.

Simba na Yanga zitakutana Jumamosi ijayo kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam na mshindi wa mechi hiyo ndiye ataongoza kwenye msimamo ambao sasa Yanga ndio kinara ikiwa na pointi 19 na Simba ni ya pili na pointi 17

Mtemi amevunja ukimya kuelekea kwenye dabi hiyo, akiwataja wachezaji hao kuwa kikwazo kwa Simba

"Simba ukabaji wao si mzuri, japo dabi haitabiriki, lakini naamini Bangala, Mayele, Aucho na Feisal watatusumbua sana," alisema Mtemi

Alisema Bangala na Aucho wana utulivu wa hali ya juu wakiwa uwanjani, hawana papara na mpira

"Wametulia wanajua wakati gani watoe pasi na iende wapi, uchezaji wao ni kama wa Lwanga japo tofauti yao ni kwamba Lwanga ana vurugu nyingi uwanjani. Aucho na Bangala wataisumbua sana Simba, hata Mayele na Feisal, Jumamosi Simba wawe makini nao sana

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
2h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
6h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
11h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
11h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
15h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’