Jumamosi pale uwanja wa Benjamin Mkapa Wananchi watakuwa na jambo lao dhidi ya watani zao Simba watakapokutana nao katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Baada ya ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii, ushindi siku ya Jumamosi ni matokeo muhimu sana kwani yataikita Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi
Lakini pia, ni matokeo ambayo yatawanyamazisha kabisa watani zao ambao hawajashinda mchezo wowote wa ligi dhidi ya Yanga katika misimu miwili iliyopita
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amewataka mashabiki wachangamkie tiketi ili kuhakikisha wanakuwepo uwanjani kwa wingi siku ya Jumamosi kuishangilia timu yao
Wakati wao wakiendelea kubishana kuhusu nembo ya Mdhamini mwenza wa Ligi (GSM) Wananchi wanaendelea kujiimarisha tayari kuwapa furaha mashabiki wao Jumamosi