Mlinzi wa kushoto wa Yanga Bryson David alionyesha kiwango bora kwenye mchezo dhidi ya Mbeya Kwanza akianza kwenye kikosi cha kwanza kwa mara ya kwanza
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi alimpumzisha Kibwana Shomari ambaye tangu kuanza kwa msimu huu ametumika kama mlinzi wa kushoto akihamishwa kutoka upande wa kulia kumpisha Djuma Shabani
Kuelekea mchezo dhidi ya Simba Jumamosi, Nabi atakuwa na mtihani wa kuamua nani amuanzishe kati ya Kibwana na Bryson
Kibwana amekuwa na faida zaidi kwenye ulinzi wakati Bryson amekuwa bora sana katika kushambulia. Ameonyesha umahiri mkubwa katika kupiga krosi

Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema nyota hao wote watapata nafasi ya kucheza kutegemeana na mahitaji ya mchezo
"Tulianza msimu tukiwa na mapungufu upande wa kushoto ndio maana tukamuhamisha Kibwana kwenye nafasi hiyo. Kibwana ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa pia kijana anayeweza kucheza maeneo tofauti tofauti uwanjani"
"Kwa sasa wote wapo kwenye ubora wa juu na tutawatumia wote katika mechi tofauti tofauti na tunaimani watatupa tunachokitaka," alisema Kaze