Mshambuliaji Amissi Tambwe ambaye alishindwa kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi baada ya kuugua malaria kali na kulazimika kurejea Dar, ameanza mazoezi jana baada ya kupona.
Mara ya mwisho kwa Tambwe kuonekana dimbani ilikuwa ni Disemba 31, 2017 kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Mbao FC ambapo Yanga ililala kwa mabao 2-0.
Kurejea kwake kumeongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji ya Yanga ambayo imepata pigo kwa kinara wake wa mabao Obrey Chirwa kufungiwa michezo mitatu baada ya kupatikana na hatia ya utovu wa nidhamu.
Naye Ibrahim Ajib aliyekosa mchezo dhidi ya Mbao akitumikia adhabu ya kadi tatu za njano, yuko tayari kuivaa Mwadui FC kesho.

ADVERTISE HERE