Kesho Jumatano, Januari 17 2018 kikosi cha Yanga kitashuka kwenye dimba la Uhuru kuumana na Mwadui FC katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 13.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amesema kikosi cha Yanga kiko tayari kuikabili Mwadui FC kesho.
Aidha, Ten amebainisha kukosekana kwa beki Abdallah Shaibu 'Ninja', Donald Ngoma na Thabani Kamusoko ambao hawako timilifu licha ya kuanza mazoezi mepesi.
Geofrey Mwashiuya naye ataukosa mchezo huo kwa kuwa ni mgonjwa huku Obrey Chirwa akikosa kwa kuwa anatumikia adhabu ya kukosa mechi tatu
Amissi Tambwe amepona malaria na leo asuuhi amefanya mazoezi hivyo huenda akatumika kwenye mchezo wa kesho kutegemea maamuzi ya benchi la ufundi.
Ten amewataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kesho kwenye uwanja wa Uhuru kuipa sapoti Yanga iliyodhamiria kuondoka na alama zote tatu ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutetea ubingwa wake.

ADVERTISE HERE