Mkurugenzi wa Sheria klabu ya Yanga Simon Patrick amewakumbusha viongozi wanaosimamia soka nchini ni vyema wakatekeleza majukumu yao kwa kufuata taratibu zilizowekwa
Jana uwanja wa Benjamin Mkapa kulitokea sintofahamu iliyopelekea Mtendaji Mkuu wa Simba Barbara Gonzalez kuzuiwa kuingia uwanjani baada ya kushindwa kufuata taratibu
Aidha Simon amesema viongozi wanapaswa kuchukua mfano ulionyeshwa na wachezaji wa Yanga na Simba kabla na baada ya mchezo jana
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Simon ameandika haya;
"Kitendo cha Wachezaji wa Yanga na Simba kukutana kabla na baada ya mchezo wa jana kupiga stori na kutabasamu kimenikumbusha kwamba mpira ni mchezo wa upendo
Viongozi tumekua chanzo cha kuleta uhasama kwenye mpira kwa kutekeleza agenda binafsi chini ya mwamvuli wa Vilabu
Kwenye mpira wetu, haijalishi wewe ni mwenyeji au mgeni wa mchezo, kumekuwa na utaratibu wa TFF kumiliki eneo la VVIP
Kwa lugha rahisi ni kwamba Klabu una kodisha na kulipia uwanja kama timu mwenyeji lakini eneo la VVIP sio lako ni la TFF/TPLB na kama vilabu tumekua tukiheshimu hili japo hatukubaliani nalo.
Klabu ya Yanga ina wajumbe wa Baraza la wadhamini 5 ambao kwa mujibu wa Katiba ni kama wamiliki wa timu kwa niaba ya Wanachama, Wajumbe wa Kamati ya Utendaji 13, CEO 1, na Wakurugenzi 5 ambao jumla ni viongozi wakuu 24 na wote wana accreditations za VVIP kwenye michezo yote ya ligi kuu, lakini accreditations hizo hazitumiki kwenye michezo ya dabi ya Kariakoo .
Yanga ina wadhamini 8 ambao kwa mujibu wa mikataba ya udhamini wanastahili kupewa VVIP tickets zisizopungua 2 kila mechi, lakini kwenye mchezo wa jana Yanga ilipewa jumla ya VVIP tickets 20 tu
Baraza la wadhamini na Wakurugenzi wote wa Yanga ambao huendesha shughuli za kila siku za Klabu tulikosa VVIP tickets lakini hakuna aliyelalamika kwa kuheshimu utaratibu wa TFF/ TPLB.
Kwenye mchezo wa ngao ya Jamii, baadhi ya Wakurugenzi nikiwemo na mimi nilizuiliwa kuingia eneo la VVIP na ticket yangu mkononi kwa kuambiwa kwamba Dr. Abbas amepunguza majina ya watu wanaostahili kuingia VVIP, kama Viongozi tulitii maelekezo hayo hatukulalamika tuliamini TFF au Dr. Abbas wana sababu za msingi.
Ifike mahali Viongozi wa mpira tukubali kwamba kuwa kiongozi hakukufanyi kuwa Mungu mtu, ni vyema kuheshimu taratibu za Viongozi wetu wa TFF/TPLB hata kama kwa upeo wako unaona hazina mashiko pengine na wao wanakuwa na sababu za msingi ambazo hawawezi kutueleza.
Hivi imagine Wangeruhusiwa wale Watoto wakakae VVIP ili hali wakurugenzi wa Yanga na Baraza la Wadhamini la Klabu ya Yanga wamekosa VVIP tickets ingeleta taswira gani kwenye soka la Tanzania? Tukiheshimiana mpira wa Tanzania utafika mbali sana"