Uongozi wa klabu ya Yanga umewashukuru mashabiki wake kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba ambao ulipigwa jana Jumamosi katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Ilikuwa siku nzuri kwa Wananchi waliofurika uwanja wa Benjamin Mkapa, walipata burudani nzuri kutoka kwa tumu yao licha ya kuwa mchezo ulimalizika kwa suluhu ya bila kufungana
"Shukrani kwa Wapenzi, Wanachama na Mashabiki wa nyumbani Dar es Salaam pamoja na Mikoa ya jirani. Shukrani za dhati pia kwa Mashabiki wetu waliosafiri kwa wingi kutoka Mikoa mbalimbali na nchi za jirani kuja kutusapoti. Hakika Hii ndo maana halisi ya timu ya wananchi," ilisema sehemu ya taarifa ya Yanga





ADVERTISE HERE