Dirisha dogo la usajili kufunguliwa Jumatano

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Dec 2021
Dirisha dogo la usajili kufunguliwa Jumatano

Usiku wa kuamkia Jumatano, Disemba 15 dirisha dogo la usajili litafunguliwa, ikiwa ni nafasi kwa klabu za ligi kuu, Championship kuboresha vikosi vyao

Wananchi wanasubiri kuona ni wachezaji gani watakongezwa katika dirisha hili

Zipo nafasi ambazo zitajazwa kulingana na Mkurugenzi wa uwekezaji GSM, Injinia Hersi Said

Kwanza ni zile nafasi mbili za nyota wa kigeni kukamilsha idadi ya wachezaji 12 walioruhusiwa na TFF

Katika nafasi hizo, nafasi moja atasajiliwa mshambuliaji ambaye atakuwa mbadala wa Yacouba Songne aliye majeruhi

Yacouba atakuwa nje kwa takribani miezi mitano, ni wazi msimu wake utakuwa umefika mwisho, Wananchi watarajie kumuona dimbani msimu ujao

Imeelezwa mbadala wake tayari yuko nchini kukamilisha usajili wake, Mcongomani Jean-Marc Mundele Makusu akitajwa kuwa chaguo la kwanza la kocha Nasreddine Nabi

Makusu kwa sasa anaitumikia DC Motema Pembe kwa mkopo akitokea klabu ya AS Vita

Msimu uliopita aliitumikia Orlando Pirates pia kwa mkopo, lakini hakuwa na nafasi ya kutosha ya kucheza baada kuwa majeruhi kwa muda mrefu

Nabi alimuhitaji Makusu kabla ya uamuzi wa kumrejesha Makambo, ilikuwa ushauri wa uongozi wa Yanga kumfuatilia nyota huyo ili kujiridhisha na uwezo wake baada ya kuwa amekaa nje kwa muda mrefu akiwa majeruhi

Yanga pia inahusishwa kumuwania kiungo wa Kimataifa wa DR Congo Fabrice Ngoma anayeitumikia klabu ya Raja Casablanca ya Morocco

Injinia Hersi ameahidi kuwa wachezaji watakaowasajili watakuwa na sifa ya kuingia katika kikosi cha kwanza moja kwa moja kama walivyofanya katika usajili uliopita

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
2h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
7h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
8h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’