Mshambuliaji wa Yanga Yacouba Songne amesema yuko salama kiafya akiendelea na matibabu ya jeraha la goti baada ya kufanyiwa upasuaji
Yacouba alipata majeraha ambayo yatamuweka nje kwa muda mrefu, ameshukuru kwa wote wanaomtakia kheri aweze kupone na kurejea uwanjani haraka
"Mimi sijambo, nawashukuru wote wanaonitia moyo, naendelea vyema na matibabu," Yacouba alisema
Juzi Jumamosi Yacouba alikosa mchezo wa kwanza wa dabi tangu aliposajiliwa na Yanga, mashabiki wengi wakiamini kama angekuwepo, hali ingekuwa ngumu zaidi kwa Simba
Katika michezo mitano aliyocheza msimu huu, Yacouba ametoa assisti mbili
ADVERTISE HERE