Vinara wa ligi kuu ya NBC, Yanga leo wanaianza kampeni ya kusaka ubingwa wa kombe la FA kwa kuikabili Ihefu Fc katika mchezo wa raundi ya tatu
Mchezo huo utapigwa kuanzia saa moja kamili usiku
Ihefu Fc ni miongoni mwa timu zinazofanya vizuri ligi daraja la kwanza (Championship) hivyo hautakuwa mchezo mwepesi
Baada ya mchezo dhidi ya Simba uliomalizika kwa suluhu ya bila kufungana Jumamosi iliyopita, Yanga ilirejea kambini Avic Town kujiandaa na mchezo wa leo
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amewataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa kuishangilia timu yao
Ametaja viingilio vya mchezo huo kuwa Mzunguuko ni Tsh 5,000/-, VIP B na C ni Tsh 10,000/- na VIP A ni Tsh 15,000/-
ADVERTISE HERE