Mkurugenzi wa uwekezaji GSM Injinia Hersi Said amesema baada ya mamlaka ya usajili wa vyama vya michezo nchini kuisajili Katiba Mpya ya Yanga, inaashiria rasmi kuwa klabu inakwenda katika mfumo mpya wa uendeshaji
Hersi amebainisha baadhi ya mabadiliko yanayokwenda kutokea katika uendeshaji wa Yanga huku akichagiza na neno 'SURE BOY'
"Safari ya mabadiliko rasmi imethibitishwa na mamlaka ya usajili wa vyama vya michezo nchini.
Hatua hii ya kuisajili KATIBA YA MABADILIKO ( 2021 ) inaashiria rasmi kuwa klabu yetu itakuwa na haya kwa uchache;
1. Umiliki wa klabu wa 51% - 49%
2. Mfumo mpya wa uongozi utakaokuwa na RAISI na MAKAMU katika klabu.
3. Kuundwa kwa kampuni mpya itakayo jumuisha YANGA na WAWEKEZAJI.
4. Kuundwa kwa bodi yenye jumla ya wajumbe 9. Wajumbe 5 kutoka YANGA na wajumbe 4 kutoka kwa wawekezaji.
5. Kufanyika uchaguzi ili kukidhi matakwa ya kikatika.
6. Kutambua gharama mpya za uanachama na huku kukiwa na kanuni mpya za kuwatambua mashabiki na mchango wao kwenye klabu yetu.
7. Upatikanaji wa mtendaji mkuu ( CEO )
Kwa uchache, hayo juu na ziada yalikuwa ni mabadiliko yaliopitishwa na wanachama katika mkutano mkuu na sasa yamepitishwa rasmi kwa usajili wa KATIBA hii ya 2021.
Kilichobaki sasa ni UTEKELEZAJI.
Pongezi kwa wote walioshiriki katika mchakato huu na historia itawakumbuka.
SURE BOYβs will like the registration of our amended constitution"