Msimu mpya wa ligi kuu ya Wanwake 2021/22, unaanza kutimua vumbi Alhamisi, Disemba 23 ambapo kinadada wa Yanga Princess wao watashuka dimbani siku ya Ijumaa kuwakabili kinadada wa Baobab Queens mkoani Dodoma
Baada ya kukosa ubingwa wa ligi hiyo kwa tofauti ya alama moja msimu uliopita, msimu huu Yanga Princess imedhamiria kutwaa ubingwa
Habari njema kwa kinadada hao ni kurejea kwa kocha wao Edna Lema ambaye anaendelea kukiandaa kikosi chake kwa ajili ya mchezo huo wa ufunguzi

ADVERTISE HERE