Kipa wa Serengeti Boys aliyeitwa Stars atua Yanga

Admin By Admin
•
11 Jul 2017
Kipa wa Serengeti Boys aliyeitwa Stars atua Yanga
Yanga SC imekamilisha idadi ya makipa watatu baada ya kumsaini na kipa wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys, Ramadhani Awam Kabwili.

Mlinda mlango huyo atakayetimiza umri wa miaka 17 Desemba 11, mwaka huu alidaka mechi zote za Serengeti Boys kwenye Fainali za Vijana Afrika chini ya umri wa miaka 17 nchini Gabon na kusifiwa mno kwa kiwango kizuri alichoonyesha.

Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amesema Kabwili amesajiliwa baada ya kuachana na makipa wao wawili wa muda mrefu, Ally Mustafa ‘Barthez’ na Deo Munishi ‘Dida’ waliomaliza mikataba yao.

Hafidh amesema Kabwili anaungana na kipa mwingine mpya, Mcameroon Youthe Rostand aliyesajiliwa kutoka African Lyon na Benno Kakolanya ambaye anakwenda kwenye msimu wa pili tangu asajiliwe kutoka Prisons ya Mbeya.

Yanga SC, mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara wameanza mazoezi leo Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kujiandaa na msimu mpya, ingawa hawakuwa na kipa mmoja baada ya Rostand na Kakolanya kutotokea, wakati Kabwili yuko na timu ya taifa ya wakubwa, Taifa Stars mjini Mwanza.

Kabwili ameitwa kwa mara ya kwanza Taifa Stars, ambayo Jumamosi itamenyana na Rwanda ‘Amavubi’ katika mchezo wa kwanza wa kuwania tiketi ya kucheza Fainali za ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), michuano inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee.

Kwa hisani ya Bin Zubeiry
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
4h ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
9h ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
13h ago
READ MORE →
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
14h ago
READ MORE →
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
14h ago
READ MORE →
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
14h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
18h ago
READ MORE →
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE →
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE →
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE →