Kilichojiri Mkutano wa Matawi Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Dec 2021
Kilichojiri Mkutano wa Matawi Yanga

1. Mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu baada ya mabadiliko ya katiba yetu ambayo imesajiliwa katika ofisi ya msajili wa vilabu vya michezo.

2. Wanachama wote wa Yanga watahakikiwa kwa kutumia fomu maalum itakayojazwa na mwanachama na kusainiwa na viongozi wa kila tawi. Hakuna mwanachama atakayesajiliwa kupitia Makao Makuu ya klabu.

3. Mwanachama atalipia 29,000/= kwa ajili ya kupata kadi ya uanachama.

4. Wanachama wote watasajiliwa kwa njia ya dijitali. Hii itamsaidia mwanachama kupata taarifa zake kupitia simu yake ya kiganjani.

5. Kila tawi litanunua kitabu chenye kurasa 100 na katiba moja kwa kiasi cha Tsh 40,000/=. Kila tawi likiishanunua hizo nyaraka litapatiwa hati ya utambulisho kuwa ni tawi rasmi.

6. Kutakuwa na usajili wa mashabiki wa klabu.

7. Hadi sasa tunayo matawi 167 ambayo yamesajiliwa klabu

UWAKILISHI WAKATI WA KUWACHAGUA VIONGOZI WA KLABU

1. Kila tawi litakuwa na wajumbe 5 ambao watashiriki mikutano mikuu yote ya klabu

2. Uchaguzi wa kila tawi, utawachagua vingozi 8 ambao ni, Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu, Katibu Msaidizi, mweka Hazina na wajumbe watatu tu.

N- Card ndio atakuwa mtengenezaji wa kadi mpya za wananchama wa Yanga Sc baada ya mfumo wa mabadiliko kuanza rasmi

Wananchi tujiandae na kuwa na kadi hizi ambazo zitakuwezesha kuingia uwanjani kuangalia mechi za Yanga pia

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
2h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
23h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’