Mkongwe Saido Ntibazonkiza watu wanaweza kumchukulia 'poa' hapa Tanzania lakini kule Burundi ni mchezaji mkubwa sana
Wananchi wa Burundi wanajua Saido ndio Messi au Ronaldo wao, kwani ni mchezaji aliyeitangaza vyema nchi hiyo Kimataifa
Saido amebainisha kuwa uwepo wake Yanga umekuwa na faida kubwa kwa mabingwa hao wa kihistoria nchini Burundi kwani Warundi wengi wanafuatilia ligi kuu ya NBC na zaidi klabu ya Yanga
Katika mahojiano na Antonio Nugaz, Afisa Mhamasishaji wa zamani Yanga, Saido amesema 'vibanda umiza' vipo Burundi na huwa vinajaa pale Yanga inapocheza
"Mimi kuwa hapa nimeshawishi Warundi wengi kushabikia Yanga. Wengi wamenunua kin'gamuzi cha Azam ili kuiangalia Yanga ikicheza. Vibanda vya kule huwa vinajaa kila mechi ya Yanga"
"Najivunia jambo hilo na zaidi najivunia kuwa mchezaji wa Yanga, timu yenye historia kubwa Tanzania," alisema Saido
Kwa sasa Saido ni mmoja wa wachezaji muhimu wa kikosi cha Yanga akifunga mabao matatu msimu huu