Kukosekana kwa 'MTN' kunavyoitesa Yanga

Muungwana wa Yanga By Muungwana wa Yanga
β€’
18 Jan 2018
Kukosekana kwa 'MTN' kunavyoitesa Yanga
Yanga imekuwa haifanyi vizuri kwa sasa. Zipo changamoto zinazoikabili klabu na miongoni mwake ni majeruhi kwa wachezaji wake muhimu.

Amissi Tambwe, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma, Papi Tshishimbi na Obrey Chirwa hawa walitegemewa kuisadia Yanga msimu huu.

Lakini ni Tshishimbi pekee aliye na msaada huku Tambwe akirejea taratibu kwenye kiwango chake baada ya kukaa nje kwa zaidi ya miezi mitano akiwa majeruhi.

Ngoma aliitumikia Yanga katika michezo mitatu ya mwanzo kabla hajaumia na kutimkia kwao Zimbabwe.

Chirwa amekuwa na majanga ya hapa na pale yanayomfanya asiwe wa kutegemewa kikosini

Kadhalika, Kamusoko naye amekuwa nje kwa muda mrefu ingawa sasa ameanza mazoezi mepesi yatakayomrejesha dimbani.

Ukiondoa safu ya ulinzi ambayo kwa kweli inastahili pongezi, Yanga imekosa mwendelezo mzuri kwenye safu ya kiungo na ushambuliaji.

Eneo hili ndilo lililoathirika sana. Misimu miwili iliyopita Yanga ilikuwa ikibebwa na eneo la kiungo na ushambuliaji

Simon Msuva ndiye aliyekuwa mpishi na mfungaji wa mabao mengi ya Yanga. Leo hayupo, bahati mbaya mbadala wake hajapatikana.

Sehemu ya kiungo iliimarishwa na Kamusoko akishirikiana na Niyonzima au wakati mwingine Kaseke.

Msimu huu Yanga imecheza michezo mingi bila ya wachezaji hao, huku wengine kama Niyonzima, Kaseke wakiwa wamehama.

Katika ushambuliaji Msuva, Ngoma, Tambwe na Chirwa walikuwa moto wa kuotea mbali. Hawa walikuwa na ligi ya kwao wenyewe kwenye upachikaji wa mabao.

Kasi ya upachikaji mabao ya Msuva, Tambwe na Ngoma ilipelekea mashabiki kuwapachika jina la 'MTN' wakiiga ule ufupisho maarufu uliotamba katika klabu ya FC Barcelona, 'MSN' Messi, Suarez na Neymar.

Msimu uliopita Ngoma alicheza mzunguuko wa kwanza tu lakini alifunga mabao nane, Msuva mabao 14, Chirwa mabao 12 na Tambwe mabao 11.

Kukosekana kwa hawa watu ni tatizo Yanga. Waliopo wanafanya vizuri lakini kutokana na uchanga wao ni dhahiri wanahitaji muda kuimarika zaidi.

Aidha, benchi la ufundi linalazimika 'kujaribu' wachezaji tofauti tofauti ili kusaka mbadala sahihi, hili ndilo linaiathiri Yanga kwa sasa

Kumekuwa na malalamiko kuwa timu inabadilika kila mechi, hilo linasababishwa na kukosekana kwa baadhi ya wachezaji muhimu. Benchi la ufundi linajaribu kupata watu sahihi katika namba sahihi.

Lwandamina na wasaidizi wake imebidi waanze upya kuisuka Yanga, pengine itachukua muda kuweza kurejesha makali yake.

Jambo la msingi nafikiri ni kuliacha benchi la ufundi liendelee kuboresha kikosi kwa kuwa yaliyotokea yako nje ya uwezo wao.

Pia Yanga kwa sasa iko kwenye mchakato wa kufanya mabadiliko ya mfumo wa uwendeshaji. Mchakato huu ukikamilika na kuiwezesha klabu kuwa na uwezo mkubwa wa kifedha, mambo mengi yatakwenda sawa.

Pengine mwishoni mwa msimu huenda tukaishuhudia Yanga ikisuka upya kikosi chake kwa kuachana na wachezaji majeruhi wa muda mrefu na wale ambao hawana msaada kwenye timu bila ya kujali ukubwa wa majina yao.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’