Kuna watu walijipachika jina la Wafanyabiashara wa mkoani Dodoma na kuwaahidi Dodoma Jiji Tsh Milioni 10 kama wangepata ushindi dhidi ya Yanga
Lakini kilichowatkea leo ni funzo kwa wengine kuwa wasijaribu kujidanganya kuwa wanaweza kutumika kuizuia Yanga kushinda ubingwa msimu huu
Kipigo cha mabao 4-0 ambacho Dodoma Jiji wamekutana nacho leo, kimefuta zile kelele za wale waliokuwa wakijipa matumaini ya uongo
Sio kwa Yanga hii! Dodoma Jiji wamechapwa na timu bora, iliyokuwa na kiwango bora pia
Feisal, Fiston Mayele, Jesus Moloko na Khalid Aucho, wameihakikishia Yanga kupata ushindi muhimu ambao unawaweka kileleni mwa msmamo wa ligi kwa tofauti ya alama nane
Sasa kazi ni kwao, TFF waendelee kuwatengenezea viporo tu, safari hii Wananchi wamedhamiria kutimiza jambo lao