Ulikuwa ni mwanzo mzuri kwa kipa wa Yanga, Abuutwalib Mshery baada ya kumaliza dakika 90 za mchezo wake wa kwanza bila kuruhusu bao
Mshery alikuwa langoni akiiongoza Yanga wakati wakiichapa Dodoma Jiji mabao 4-0 katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Yanga ililazimika kuharakisha usajili wake na kupata vipali vyote siku moja tu baada ya kumsajili kutoka Mtibwa Sugar
Ni baada ya Djigui Diarra kuelekea Cameroon kwenye majukumu ya timu ya Taifa ya Mali katika michuano ya Afcon 2021
Ulikuwa usiku mzuri kwake, kwani licha ya kuwa kwenye presha kubwa ya kufanya vizuri, Mshery hakuwaangusha Wananchi
Katika mchezo huo mashabiki walilinganisha kila tukio alilofanya dhidi ya Djigui Diarra
Ni aina ya mlinda lango ambaye Yanga ilimuhitaji na hakika amekuwa na mwanzo mzuri