Nabi na mpango wa kuimarisha nyota wa ndani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Jan 2022
Nabi na mpango wa kuimarisha nyota wa ndani

Ameandika Mkurugenzi wa Sheria klabu ya Yanga, Wakili Msomi Simon Patrick;

Siri ya Coach Nabi na Kaze na Wazawa! Coach Nabi na Kaze wamekuja na philosophy itakayolisaidia taifa na timu ya taifa miaka ya hivi karibuni.

Wamekuwa wakifatilia kwa makini mechi zote za ligi kuu na daraja la kwanza ili kuviona vipaji, na pale watakapojiridhisha huwashawishi viongozi kuchukua vipaji hivyo.

Coach Nabi mkakatati wake ni kwamba kila namba yenye mchezaji wa kigeni lazima iwe na mchezaji mzawa kama succession plan.

Kinachofata huwapa mafunzo maalumu na kuwaandaa kupambania namba huku akiwapa fursa kidogo kidogo, atakayeweza kumshawishi basi anajipatia namba ya kudumu.

Binafsi nimependa sana huu mpango wa Mwalimu, na ni fursa kwa wachezaji wa kizawa kutumia changamoto hii kujiendeleza.

Ujumbe wangu kwa wachezaji wote wa kitanzania, Mpira ni Biashara, hakuna timu itakayokutaka kwa uraia wako, bali kipaji chako, mkiweza kuwatumia wageni kujipima na kuweka juhudi za kupambana zaidi, mnajifungulia soko nje ya mipaka ya Tanzania.

Leo hii kuna wachezaji wameridhika kusifiwa na kufananishwa na wageni, bila kujua kitendo cha mchezaji kuvuka mpaka wa nchi yake kwenda nchi nyingine ni mafanikio makubwa kwa mchezaji na taifa kwa ujumla kuliko sifa na utukufu anaopewa mchezaji nyumbani kwake.

Mdogo wangu Denis Nkane Coach Nabi hajakuchagua kwa bahati mbaya, una kitu mguuni, mafanikio yako kwenye mpira unayo wewe mwenyewe, wewe ndio mchezaji mdogo kuliko wote kwenye ligi (Miaka 19) una mengi ya kutuonesha waTanzania.

Nakutakia kila lenye heri kwenye maisha yako mapya, karibu sana kwa Wananchi timu yenye mashabiki wenye upendo wa hali ya juu kuwahi kutokea

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
9h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’