Wachezaji wa Yanga wamepewa mapumziko ya siku tatu kabla ya kuelekea visiwani Zanzibar kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi
Aidha kutegemea na mahitaji ya kocha Nasreddine Nabi na benchi lake la ufundi, baadhi ya wachezaji huenda wakapumzishwa kushiriki Mapinduzi Cup ili kuwapa nafasi nyota wengine ambao hawakutumika sana
Khalid Aucho, Fiston Mayele ni miongoni mwa wachezaji ambao wametumia mapumziko hayo kusafiri kuziona familia zao

Yanga itacheza mechi ya kwanza Januari 05 dhidi ya Taifa ya Jan'gombe mchezo utakaopigwa uwanja wa Amaan, saa mbili usiku
ADVERTISE HERE