Kiungo wa Yanga Zawadi Mauya amesema Kocha Mkuu wa timu hiyo Nasreddine Nabi ndio sababu ubora anaoonyesha kwenye kikosi cha Yanga
Mauya amekuwa katika kiwango bora kwenye michezo minne iliyopita ambapo amecheza zaidi ya dakika 360
Mauya amefichua kuwa Nabi amekuwa akiwapa mazoezi maalum viungo ili kuhakikisha wanafanya vile wanapaswa
"Mwalimu anahitaji utulivu mkubwa eneo la kiungo . Mara nyingi hutupa mazoezi ya ziada sie viungo kwakuwa ndio moyo wa timu"
"Nafurahi kuona timu inafanya vizuri nami nafanya vyema. Kuna mengi ya kujifunza kuufikia ubora ambao kocha anauota kwa hii klabu yetu .
"Kikubwa kujituma, sapoti ya mashabiki na viongozi, nina imani tutafanya vyema sana msimu huu," alisema Mauya
ADVERTISE HERE