Kaimu Mtendaji Mkuu wa Yanga Senzo Mazingisa amesema baada ya Serikali kuipitisha Katiba Mpya ya Yanga, ndani ya miezi sita watakamilisha mabadiliko kulingana na Katiba Mpya
Senzo amesema wameanza na zoezi la kusajili Wananchama, baadae itafanyika tathmini ya thamani ya klabu kabla ya kuwaalika Wawekezaji
Senzo amesema Yanga ndio klabu pekee ambayo mchakato wake wa Mabadiliko Serikali imeupitisha na kuukubali
"Sisi tumeendesha Mchakato wetu wa Mabadiliko kwa uwazi. Ndio maana Serikali imeupitisha na kuuridhia"
"Hakuna klabu ambayo mchakato wake umepitishwa na Serikali zaidi ya Yanga kama ipo nitolee mfano," alifunguka Senzo katika mahojiano na Clouds TV
"Tumepewa miezi 6 kuhakikisha yote tuliyoandika kwenye Katiba kuhusu Mabadiliko yanafanyika. Sasa tupo kwenye mchakato wa kutafuta thamani ya klabu halisi, huku tunasajili Wanachama, baada ya hapo sasa tutaita Wawekezaji waje kuwekeza kulingana na thamani ya Klabu yetu"
"Tunafanya na tutafanya kila kitu kwa uwazi na hii ni mara ya kwanza Mabadiliko yanafanywa uwazi na kila mtu anatakiwa kujua"