Kiungo mshambuliaji wa Yanga Saido Ntibazonkiza tayari amewasili visiwan Zanzibar kuungana na kikosi kuelekea mchezo wa nusu fainali kombe la Mapinduzi dhidi ya Azam Fc
Saido alikuwa miongoni mwa wachezaji waliopewa mapumziko baada ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Dodoma Jiji
Nyota huyo anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kitakachoikabili Azam Fc kesho Jumatatu
Wachezaji wengine waliotarajiwa kutua visiwani Zanzibar leo ni pamoja na Khalid Aucho, Yannick Bangala, Mukoko Tonombe, Djuma Shabani, Fiston Mayele pamoja na kocha mkuu Nasreddine Nabi
ADVERTISE HERE