Kiungo fundi wa Yanga Khalid Aucho amerejea nchini kujiunga na kikosi cha Yanga kinachoshiriki michuano ya kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar
Wakati Aucho akitua, kiungo Mukoko Tonombe na mlinzi Djuma Shabani nao wanatarajiwa kuwasili nchini leo
Mukoko, Djuma na Yannick Bangala walikuwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya DR Congo kilichokuwa kimeweka kambi Misri
Bangala alirejea nchini jana na anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi kitakachoikabili Azam Fc baadae leo katika mchezo wa nusu fainali kombe la Mapinduzi
ADVERTISE HERE