Yanga imeondoshwa kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi kwa mikwaju ya penati 9-8 baada ya mchezo kumalizika kwa suluhu ya bila kufungana
Ulikuwa mchezo mgumu ambao Yanga haikutengeneza nafasi nyingi kama ilivyozoeleka
Piga nikupe katika mikwaju ya penati, ikaishia kwa Yassin Mustafa kukosa na kuwapa nafasi Azam Fc kusonga mbele
Yanga inarejea Dar sasa kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union ambao utapigwa Januari 16 katika uwanja wa Mkwakwani
ADVERTISE HERE