Jana Yanga imeondoshwa kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi, wakipoteza mchezo wa nusu fainali dhidi ya Azam Fc kupitia mikwaju ya penati
Yanga ilikwenda Zanzibar ikiwa na melengo ya kutetea ubingwa wa michuano hiyo ambao walitwaa mwaka jana
Hata hivyo haikuwa bahati kwa Wananchi ambao sasa wanarejea jijini Dar es salaam kujiandaa na mikiki mikiki ya ligi kuu
Januari 16, Yanga inakabiliwa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union ambao utapigwa uwanja wa Mkwakwani
Moja ya viwanja vigumu kwa Yanga kuondoka na alama zote tatu katika misimu ya hivi karibuni
Hivyo Wananchi tunapaswa kusahau yaliyotokea visiwani Zanzibar na kuunganisha nguvu kuelekea mchezo huo
Ubingwa wa ligi kuu ndio hitaji la kwanza kwa Yanga, hivyo nguvu kubwa inapaswa ielekezwe huko
Naamini wachezji watarejea kwenye ligi wakiwa na nguvu mpya, kuendeleza pale walipoishia mwaka 2021