Yanga imepania kumaliza unyonge Tanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Jan 2022
Yanga imepania kumaliza unyonge Tanga

Uwanja wa Mkwakwani umekuwa mgumu kwa Yanga kupata matokeo katika misimu ya hivi karibuni

Msimu uliopita Coastal Union ilikuwa timu ya kwanza kuifunga Yanga katika mchezo ambao ulipigwa hapo Mkwakwani

Msimu huu Yanga imedhamiria kumaliza unyonge, Wananchi wakipania kushinda mchezo utakaopigwa Jumapili, Januari 16

Baada ya kurejea kutoka Zanzibar, Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi aliagiza vijana wake waelekee moja kwa moja kambini kujiandaa na mchezo huo pamoja na ule unaofuatia dhidi ya Polisi Tanzania ambao utapigwa Januari 23 kwenye uwanja wa Ushirika, Moshi

Polisi Tanzania pia ilichangia kuvuruga hesabu za ubingwa kwa Yanga msimu uliopita wakiwalazimisha mabingwa hao wa kihistoria sare ya bao 1-1

Meneja wa Yanga Hafidh Saleh amesema wanaendelea vyema na maandalizi ya michezo hiyo ambapo ni wachezaji watano tu wanaokosekana

Wachezaji hao ni Djigui Diarra(Afcon), Kibwana Shomari na Abdallah Shaibu waliosafiri Tunisia kwa ajili ya matibabu

Pia wamo Yacouba Songne na Denis Nkane ambaye alipata majeraha kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar

Nkane anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki nne

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
4h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
8h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’