Nitajifunza mengi kutoka kwa Diarra - Mshery

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Jan 2022
Nitajifunza mengi kutoka kwa Diarra - Mshery

Mlinda lango wa Yanga Abultwalib Mshery amesema anaamini atajifunza mengi kutoka kwa Djigui Diarra ambaye ndiye kipa namba moja wa Yanga

Mshery amesajiliwa na Yanga katika dirisha dogo la usajili akichukua nafasi ya Ramadhani Kabwili ambaye mkataba wake umemalizika

Aidha ujio wake ulikuwa maalum kuwa mbadala wa Diarra ambaye anakabiliwa na majukumu ya Kimataifa akiwa na Mali inayoshiriki michuano ya Afcon 2021 huko Cameroon

Mshery alianza katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Dodoma Jiji akipata cleansheet yake ya kwanza akiwa na Yanga katika mchezo ambao Wananchi waliibuka na ushindi wa mabao 4-0

Pia alidaka mechi zote tatu za michuano ya kombe la Mapinduzi isipokuwa mikwaju ya penati katika mchezo dhidi ya Azam Fc

Mshery amesema anajisikia faraja kufanya kazi na Diarra, mlinda lango mwenye uzoefu mkubwa wa michuano ya Kimataifa

"Nimefurahi kuja kufanya kazi na Diarra kwani nafahamu ni kipa mzuri ambaye ana uzoefu mkubwa wa michuano ya Kimataifa. Pia amefanya vizuri katika michezo yote aliyodaka hapa Yanga"

"Kwangu mimi itakuwa nafasi nzuri kujifunza mambo mengi kutoka kwake, naamini kufanya kazi nae nitaimarika na kuwa bora zaidi," alisema Mshery katika mahojiano na mhamasishaji wa Yanga, Haji Manara

Mshery anatarajiwa kuwa langoni siku ya Jumapili kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union ambao utapigwa uwanja wa Mkwakwani

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
3h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’