Wakati Yanga ikielekea mkoani Tanga ambapo siku ya Jumapili, Januari 16 inakabiliwa na mchezo wa ligi kuu ya NBC dhidi ya Coastal Union, Kocha Mkuu wa vinara hao wa ligi Nasreddine Nabi amerejea kutoka Ubelgiji
Nabi aliondoka nchini baada ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Dodoma Jiji uliopigwa Disemba 31, 2021 kwa ajili ya mapumziko ya siku chache
Sasa atakiongoza kikosi chake katika mchezo dhidi ya Coastal Union ambao Yanga imepania kumaliza ukame wa ushindi katika uwanja wa Mkwakwani wakipata ushindi kwa mara ya mwisho mwaka 2015
ADVERTISE HERE