Dirisha dogo la usajili ambalo lilifunguliwa Disemba 16 2021, linatarajiwa kufungwa kesho Jumamosi, Januari 15 2022, saa 5:59 usiku
Pamoja na kusajili wachezaji wanne wa ndani, Abultwalib Mshery, Denis Nkane, Abubakar Salum na Crispine Ngushi, Yanga ilikuwa ikihusishwa na nyota kadhaa wa kigeni
Kaimu Mtendaji Mkuu wa mabingwa hao wa kihistoria Senzo Mazingisa amesema wanaweza kukamilisha usajili wa mchezaji mmoja wa kigeni
Senzo amedokeza kuwa wako katika hatua za mwisho kukamilisha usajili huo ambao sio tu utatikisa nchi, bali pia utakiongezea thamani kikosi cha Yanga
Senzo amebainisha kuwa wako katika hatua za mwisho kukamilisha masuala ya mikataba kabla ya kutangaza usajili huo
ADVERTISE HERE