Yanga iliahidi kutambulisha usajili wa nyota wa Kimataifa kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa hapo jana
Hata hivyo tukio hilo halikutokea, kuna waliokesha kusubiri taarifa hiyo pasipo mafanikio
Afisa Mhamasishaji wa Yanga Haji Manara amesema ilikuwa katika mipango yao kufanya tukio hilo mkoani Tanga kabla ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union ambao utapigwa uwanja wa Mkwakwani baadae leo
Manara amesema watatambulisha wachezaji WAWILI na sio mmoja!
Amewataka mashabiki wa Yanga mkoani Tanga kuwahi mapema uwanjani kwa ajili ya tukio hilo alilolifananisha na WIKI YA MWANANCHI ndogo
Tukio hilo pia litarushwa mbashara na Azam TV
Hii itakuwa 'suprise' ya aina yake....!
ADVERTISE HERE